DAR- Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limewaalika wananchi na wateja wake na kutembelea mradi wa makazi wa Kawe 711 jijini Dar es Salaam ili kupata maelezo zaidi kuhusu mradi huo na kujionea nyumba zilizojengwa.
Muonekano wa nyumba za NHC katika Mradi wa 711 uliopo Kawe, Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.Ziara hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja, yanayolenga kuimarisha mawasiliano kati ya shirika wananchi na wateja wake, pamoja na kuwapatia taarifa zinazohusu huduma na fursa za ununuzi wa nyumba.
Kwa mujibu wa taarifa ya NHC, wawakilishi wa benki zinazoshirikiana na shirika hilo pia watakuwepo katika eneo la mradi kutoa elimu kuhusu huduma za mikopo ya nyumba na kuwaelekeza wananchi namna ya kunufaika na huduma hizo.
Aidha, wawakilishi wa NHC watakuwa katika mradi wa Kawe 711 kuanzia Oktoba 12 hadi 16, 2026, saa mbili asubuhi hadi saa kumi na moja jioni.
Wananchi wanahimizwa kutumia fursa hiyo kutembelea mradi huo, kupata ufafanuzi kuhusu nyumba zinazopatikana na kujifunza zaidi kuhusu miradi mingine inayotekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa.
Tags
Dar es Salaam
Habari
Kawe
Makazi
Mikopo ya Nyumba
NHC
Nyumba Kawe 711
Shirika la Nyumba la Taifa
Wiki ya Huduma kwa Wateja