Rais Dkt. Mwinyi awasili nchini Qatar kwa ziara ya kikazi

DOHA-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hamad jijini Doha, Qatar, tarehe 07 Oktoba, 2026 kwa ziara ya kikazi.
Ziara hiyo inalenga kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kiuchumi kati ya Zanzibar na Qatar, pamoja na kufungua fursa mpya za uwekezaji na maendeleo kwa Zanzibar.

Akiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hamad, Rais Dkt. Mwinyi amepokelewa na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Qatar, Mhe. Habibu Awesi Mohamed.

Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha diplomasia ya kiuchumi, kuvutia uwekezaji na kukuza ushirikiano wa kimkakati kwa manufaa ya wananchi wa Zanzibar

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here