DOHA-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, tarehe 08 Oktoba 2026, ameeleza fursa za uwekezaji zilizopo Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, hususan katika sekta za utalii, hoteli, makaazi na huduma za wageni, wakati alipokutana na mfanyabiashara wa kimataifa na Rais wa Makampuni ya Alfardan, Bw. Omar Hussain Alfardan jijini Doha, Qatar.
Mazungumzo hayo yamelenga kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kuvutia uwekezaji utakaosaidia kukuza uchumi na kuongeza ajira.Aidha, Rais Dkt. Mwinyi ametembelea The Pearl Island, mradi mkubwa wa makaazi, biashara na huduma, ambako amefahamishwa kuhusu uendelezaji, usimamizi na fursa za uwekezaji katika mradi huo.
Tags
Alfardan Doha
Dkt.Hussein Ali Mwinyi
Doha na Zanzibar
Fursa Zanzibar
Kimataifa
Qatar na Zanzibar










