Real Madrid Foundation kujenga Akademia ya Soka Zanzibar, Roberto Carlos akutana na Rais Mwinyi

MADRID-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema ushirikiano kati ya Real Madrid Foundation na Unicorn Zanzibar Sports Limited utafungua fursa kwa vijana wa Zanzibar kukuza vipaji vya soka, kujenga nidhamu na kuimarisha maadili kupitia mafunzo yanayozingatia viwango vya kimataifa.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo Oktoba 13, 2026 jijini Madrid nchini Uhispania wakati wa hafla ya utiaji saini wa Hati ya Makubaliano inayolenga kuanzisha programu maalumu za mafunzo ya soka kwa vijana, zitakazofuatwa na kuanzishwa kwa akademia ya kudumu katika viwanja vya michezo Zanzibar.

Katika hafla hiyo, Rais Dkt. Mwinyi amepokea jezi ya timu ya Real Madrid kutoka kwa Roberto Carlos, mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil na Balozi wa Real Madrid, pamoja na Julio González Ronco, Mkurugenzi wa Real Madrid Foundation.
Tukio hilo limekuwa sehemu ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano katika kukuza michezo na vipaji vya vijana Zanzibar.

Amesema, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeendeleza zaidi ya viwanja 30 vya mpira wa miguu na itaendelea kuwekeza katika miundombinu ya michezo, maarifa na mifumo itakayowawezesha vijana kufikia uwezo wao.

Aidha, amesisitiza kuwa mafanikio katika michezo yanahitaji vipaji, nidhamu, elimu na makocha wenye ujuzi na weledi.
Rais Dkt. Mwinyi amekamilisha ziara yake ya kikazi nchini Uhispania na leo anaelekea nchini Armenia kushiriki Mkutano wa Viongozi wa PIN (PIN Leaders Summit), ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake iliyoanzia Doha, Qatar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here