Serikali: Miradi ya maji inajengwa vijiji 400, mpango unaendelea

DODOMA-Serikali imejipanga kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma ya majisafi, salama na yenye kutosheleza. Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amesema hayo jana katika kikao na Menejimenti ya Sekta ya Maji jijini Dodoma.
Ameainisha kuwa, mpango wa kufikisha maji katika vijiji ambavyo havijapata miundombinu umeanza na kasi iongozwe zaidi ambapo hivi sasa vijiji 400 katika mikoa mbalimbali vinajengewa miradi miongoni mwa vijiji 1,575. Kazi hiyo inafanyika kwa awamu.

Amesema, yapo mambo ambayo amebaini yanahitaji suluhu ya haraka katika ukaguzi wa miradi aliyofanya, hivyo amewapa kazi wataalam wa maeneo hayo katika siku zisizozidi 30 kupata majibu ili wananchi waanze kunufaika na miradi ya maji.
Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiongoza kikao cha Menejimenti ya Sekta ya Maji jijini Dodoma jana.
Mhe. Aweso, kuhusu uhaba wa maji katika baadhi ya maeneo ya miji nchini ametaka kufanyika kwa mpango wa dharura wa kuleta ahueni kwa wateja na mgao ukifanyika uwe wa uhalisia na muda wa kutosha.

Amesema, maeneo korofi yote yanatambulika hivyo ni lazima kuyapa muarobaini ili kuwapa wateja wa maji unafuu wa kupata huduma hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri akizungumza jana jijini Dodoma katika kikao cha kikao na Menejimenti ya Sekta ya Maji kilichoongozwa na Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here