Ushirikiano Tanzania na Uingereza waacha historia Mkutano wa IPU

ARUSHA-Historia inaonesha kwa miaka arobaini (40) iliyopita Bunge la Uingereza limekuwa likishiriki katika Mikutano ya Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) katika nafasi ya uwakilishi hata hivyo, katika mkutano wa 153 ambapo Tanzania imekuwa mwenyeji wa mkutano huo Uingereza haijatuma uwakilishi isipokuwa Spika wa Bunge la Wawakilishi (House of Commons), Sir Lindsay Hoyle anashiriki mkutano huo.
Sir LindsayHoyle, aliwasili jijini Arusha na kupokelewa na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Geneva-Uswisi, Mhe. Dkt. Abdallah Possi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tarehe 3 Oktoba, 2026 kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaofanyika kuanzia tarehe 5 hadi 9 Oktoba, 2026 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC).

Ushiriki wa Sir Lindsay Hoyle unaleta somo kubwa kwa washiriki wa mkutano huo na dunia kwa ujumla kuelewa kuwa, Tanzania inaendelea kusonga mbele katika nyanja za kimataifa.
Pia ni ishara ya kuimarika kwa ushirikiano wa kihistoria kati ya mataifa hayo mawili ulioasisiwa zaidi ya miaka 60 iliyopita, ukihusisha sekta za biashara na uwekezaji, madini, elimu, miradi ya maendeleo, diplomasia na utamaduni.

Akizungumza na vyombo vya habari Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu ameeleza kuwa Tanzania imejijengea jina kubwa duniani kwa kuwa mwenyeji wa mkutano huo sambamba na kupendekezwa na Spika wa Uingereza kuongoza mkutano wa 153 wa IPU.
Aidha, pendekezo la Mhe. Zungu kuongoza mkutano wa 153 liliwasilishwa na Spika wa Uingereza na kuungwa mkono na wajumbe wa mkutano huo.

Hata hivyo, Spika Hoyle aliwasilisha pendekezo hilo kufuatia urafiki wa muda mrefu na wa kihistoria kati ya Tanzania na Uingereza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here