Waziri Kikwete aridhishwa na ujenzi wa TPSC Kampasi ya Tanga

NA VERONICA MWAFISI

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amekagua maendeleo ya ujenzi wa wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Kampasi ya Tanga na kuupongeza uongozi wa chuo hicho kwa usimamizi mzuri.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (aliyenyoosha mkono) akisisitiza jambo wakati akikagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) kilichopo Kata ya Maweni, Kange mkoani Tanga.

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa mradi huo, Mhe. Kikwete amesema anafarijika na hatua nzuri aliyoiona ya ujenzi huo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Viongozi na Watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) Mkoa wa Tanga mara baada ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Chuo hicho kilichopo Kata ya Maweni, Kange mkoani Tanga.

"Sisi ndani ya Serikali tunajua umuhimu wa jengo hili, sio pambo bali tunataka kuona majengo haya yanakuwa kitovu cha kutoa elimu katika Mkoa huu wa Tanga,"Mhe. Kikwete ameongeza.

Amesema, ni matamanio ya Serikali kuona ujenzi huo unakamilika kwa wakati kama ilivyopangwa ili kufikia malengo yaliyowekwa.
Mwonekano wa jengo la mradi wa ujenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) Kampasi ya Tanga.

“Natamani kuona mwezi Mei 2027 jengo liwe limekamilika na kuanza kutumika ili pia tuweze kuendelea na ujenzi wa majengo mengine ndani ya Kampasi hii,"amesema Mhe. Kikwete.

Amemsihi Mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi kuendelea kuifanya kazi hiyo vizuri zaidi ili kukwepa kadhia ya kubadilisha Mkandarasi mwingine pale ambapo watashindwa kufanya kama ilivyofikiwa.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Kikwete kuzungumza, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Mhe. Gilbert Kalima aliishukuru Serikali kwa kuona umuhimu wa kujenga majengo ya Chuo cha Utumishi wa Umma katika mkoa huo.
Mkurugenzi wa Kampasi ya Tanga ya Chuo cha Utumishi wa Umma, Bi. Zawadi Rashid akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) mara baada ya Waziri huyo kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa chuo hicho kilichopo Kampasi ya Tanga.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) akijadili jambo na Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Dkt. Ernest Mabonesho (kulia) mara baada ya Waziri huyo kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) kilichopo Kampasi ya Tanga.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wakwanza kushoto) akisisitiza jambo wakati akikagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) kilichopo Kata ya Maweni, Kange mkoani Tanga.
Kaimu Katibu Mkuu-UTUMISHI ambaye ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa kwanza kushoto) kuzungumza na Viongozi Watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) Mkoa wa Tanga mara baada ya Waziri huyo kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Chuo hicho kilichopo Kata ya Maweni, Kange mkoani Tanga.
Sehemu ya Wataalam wa ujenzi wanaojenga Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) kilichopo Kampasi ya Tanga wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete alipokuwa akizungumza nao mara baada ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma kilichopo Kampasi ya Tanga.
Sehemu ya Wataalam wa ujenzi wanaojenga Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) kilichopo Kampasi ya Tanga wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete alipokuwa akizungumza nao mara baada ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma kilichopo Kampasi ya Tanga.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa pili kutoka kushoto) akipata maelezo ya mradi wa ujenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) ulipofikia wakati alipotembelea mradi huo uliopo Kata ya Maweni, Kange mkoani Tanga.

Naye Kaimu Katibu Mkuu-UTUMISHI ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Bi. Prisca Lwangili amemshukuru Waziri Ridhiwani kwa mipango mizuri na namna anavyofanya ufuatiliaji wa mambo mbalimbali ikiwemo maendeleo ya ujenzi wa chuo hicho.

Akiwasilisha taarifa fupi ya maendeleo ya mradi wa ujenzi huo, Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Dkt. Ernest Mabonesho amesema ujenzi wa chuo hicho ukikamilika unatarajiwa kuchukua jumla ya wanafunzi 2,000.

Dkt. Mabonesha amemshukuru Mhe. Kikwete kwa kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara na kuwahimiza utekelezaji wa majukumu yao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here