Waziri Mchengerwa kuzindua Awamu ya Pili ya Bima ya Afya kwa Wote Mtwara

NA GODFREY NNKO,
Mtwara

WAZIRI wa Afya, Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa anatarajiwa kuzindua rasmi Awamu ya Pili ya Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote kesho Alhamisi, Oktoba 22, 2026 katika Uwanja wa Sabasaba mkoani Mtwara.
Waziri wa Afya Tanzania, Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa.

Uzinduzi huo utafanyika kuanzia saa 3:00 asubuhi, huku Waziri Mchengerwa akitarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.

Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote ni sehemu ya juhudi za Serikali za kupanua upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi, bila kujali hali zao za kiuchumi.

Lengo ni kuwawezesha Watanzania kupata matibabu kwa urahisi na kwa gharama nafuu, huku wakipunguza vikwazo vya kifedha vinavyoweza kuwazuia kupata huduma hizo.

Utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote ulianza rasmi Januari 26, 2026, ukiwa na lengo la kuweka msingi wa upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi kwa kuzingatia uwezo wao wa kumudu gharama za matibabu.

Awamu ya Pili ya mpango huo inafuatia utekelezaji wa awamu ya kwanza na inalenga kupanua wigo wa wananchi watakaonufaika na bima hiyo, sambamba na kuboresha upatikanaji na utoaji wa huduma katika vituo vya afya nchini.

Vilevile, uzinduzi huo unatarajiwa kuwa hatua nyingine katika utekelezaji wa mpango huo unaolenga kuongeza fursa za wananchi kupata huduma za afya na kupunguza changamoto zinazotokana na gharama za matibabu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here