NA DIRAMAKINI
WIZARA ya Fedha Tanzania imetoa rai kwa wananchi na watumishi wote kuendelea kukataa rushwa wanapofuatilia mafao yao ya pensheni.
Kupitia ujumbe wake leo, Wizara imesisitiza kuwa, pensheni ni haki ya mwananchi na si fadhila, hivyo hakuna sababu ya kutoa rushwa ili kupata stahiki hiyo.
"Kataa Rushwa, Linda Kipato Chako cha Uzeeni," Wizara imesisitiza katika kampeni yake ya kuelimisha umma kuhusu haki za wastaafu.
