Na Mwandishi Wetu| New Delhi India
NOVEMBA 27,2026 jijini New Delhi India, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini India, Mhe. Anisa Mbega alikutana na kusalimiana na Waziri Mkuu wa India, Mhe. Narendra Modi.
Mheshimiwa Modi alikutana na Mawaziri wa Mambo ya Nje kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Mwambao wa Bahari ya hindi (IORA) ambao walikuwa nchini humo kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 25 wa Baraza la Mawaziri la IORA uliofanyika Novemba 27, 2026 nchini humo.
Mhe. Balozi Anisa Mbega alimwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo katika mkutano wa IORA.



