Jaji mstaafu Eusebia Munuo amtembelea Jaji Mkuu Masaju

DODOMA- Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Eusebia Nicholas Munuo tarehe 17 Novemba, 2026 alimtembelea Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju na kupata fursa ya kufanya naye mazungumzo mafupi ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.

Matukio katika picha, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Eusebia Munuo alipotembelea Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju tarehe 17 Novemba, 2026 Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju akisalimiana na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Eusebia Nicholas Munuo (kulia) alipomtembelea Jaji Mkuu ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma tarehe 17 Novemba, 2026. Kushoto ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani.
Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Eusebia Nicholas Munuo (kulia) akisaini kitabu cha wageni alipomtembelea Jaji Mkuu ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma tarehe 17 Novemba, 2026.
Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Eusebia Nicholas Munuo (kushoto) akifanya mazungumzo na Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju ofisini kwa Jaji Mkuu Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma tarehe 17 Novemba, 2026.
Mazungumzo yakiendelea. Kushoto ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania na Amidi wa Mahakama hiyo, Mhe. Augustine Mwarija.
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Eusebia Nicholas Munuo.
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Eusebia Nicholas Munuo (wa pili kushoto). Wa kwanza kushoto ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania na Amidi wa Mahakama hiyo, Mhe. Augustine Mwarija na wa kwanza kulia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Lushoto, Mhe. Dkt. Paul Kihwelo.
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju (kulia) akiagana na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Eusebia Nicholas Munuo.(Picha na MARY GWERA, Mahakama-Dodoma).
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju akizindua Kitabu cha historia ya Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Eusebia Nicholas Munuo kinachoitwa ‘JUSTICE EUSEBIA MUNUO: A Trailblazer in the Legal Profession in Tanzania’ leo tarehe 17 Novemba, 2026 kwenye ukumbi wa mikutano Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania-Dodoma. Wanaoshuhudia zoezi hilo kushoto ni, Jaji Mstaafu, Mhe. Munuo na kulia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Lushoto, Mhe. Dkt. Mary Levira.

Kadhalika, Mhe. Munuo aliwasili Makao Makuu ya Mahakama ili kushiriki katika Hafla ya Uzinduzi wa Kitabu chake kiitwacho JUSTICE EUSEBIA MUNUO: A Trailblazer in the Legal Profession in Tanzania” kilichozinduliwa na Jaji Mkuu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here