Makamu wa Rais Ndejembi afanya mazungumzo na Rais Museveni

ENTEBBE- Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Bomba la Mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani, Tanga Tanzania.
Mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu ya Entebbe nchini Uganda, yanalenga kuendelea kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Uganda katika miradi ya kimkakati ikiwemo sekta ya mafuta na gesi.
Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe, Balozi wa Tanzania nchini Uganda Mhe. Meja Jenerali Marco Gaguti, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshughulikia mafuta na gesi Dkt. James Mataragio, Kamishna wa Mafuta na Gesi Bw. Goodluck Shirima pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Mussa Makame.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here