Mao na Hincha wa Kijiji cha Waranga wilayani Hanang' hatiani kwa kosa la kughushi

Na DIRAMAKINI 24| Manyara

WASHTAKIWA Amani Gabriel Mao na Abdallah Hassan Hincha wametiwa hatiani katika Mahakama ya Wilaya ya Hanang’ mkoani Manyara kwa kosa la kughushi kinyume na kifungu cha 333, 335(a) na 337 vya Kanuni ya Adhabu (Sura ya 16).
Ni kupitia shauri la uhujumu uchumi namba 20806/2026 ambapo uamuzi umetolewa mahakamani hapo Novemba 17, 2026.

Washtakiwa kwa pamoja walighushi muhtasari wa kikao cha Halmashauri ya Kijiji cha Waranga na kutoa fedha benki kiasi cha TZS 3,300,000.

Akisoma hukumu hiyo, Mheshimiwa Arnold Kileo, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Hanang’ amewatia hatiani washtakiwa Amani Gabriel Mao
ambaye alikuwa Kaimu Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Waranga.

Sambamba na Abdallah Hassan Hincha ambaye alikuwa Mwenyekiti wa kijiji hicho baada ya washtakiwa kuingia makubaliano na ofisi ya DPP na kukiri kosa.

Kwa pamoja, washtakiwa wameamuriwa kumfidia mhanga ambaye ni Halmashauri ya Kijiji cha Waranga kiasi cha TZS 3,300,000/= na kila mmoja kulipa faini ya kiasi cha TZS. 100,000 au kutumikia adhabu ya kifungo cha miezi sita gerezani.

Washtakiwa wamelipa faini na kurudisha kiasi cha TZS. 3,300,000 katika akaunti ya mhanga.

Shauri hilo lilikua linaendeshwa na waendesha mashtaka wa TAKUKURU Bw. Daudi Kingazi, Bi. Neema Gembe na Bi. Catherine Ngessy.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here