Naibu Waziri wa Maji akagua mitambo ya uzalishaji maji Ruvu Juu na Ruvu Chini

Na Mwandishi Wetu| Ruvu

MITAMBO ya kuzalisha maji ya Ruvu chini na Ruvu juu imekaguliwa kubaini hali ya uzalishaji wa maji yanayoenda kwa wateja baada ya uwekezaji mkubwa wa serikali wa takriban Bilioni 16 za pampu mpya.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Kundo Andrea Mathew (Mb) amekagua mitambo hiyo ili kujua hatua zinazochukuliwa kutatua changamoto ya uhaba wa maji katika baadhi ya maeneo.
Amesisitiza utekelezaji wa maelekezo ikiwamo kuhakikisha kila eneo linapata majisafi kuendana na mgao, na endapo changamoto inatokea ifanyiwe kazi ndani ya muda mfupi na na mgao usiruke eneo lililopangwa.

Naibu Waziri Kundo amesisitiza uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali matokeo yake ni maji kufika kwa walaji, ambao ni wananchi.
Ameainisha kuwa Serikali imenunua pampu mpya nane kwa ajili ya kuongeza nguvu ya mitambo hiyo ambayo ilianza kazi miaka ya 70 na kuboreshwa mwaka 2014.

Uwekezaji huo ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuongeza uwezo wa uzalishaji na kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi wa Dar es Salaam.
Katika ukaguzi huo, Naibu Waziri Kundo ameambatana na Wabunge wa Majimbo ya Segerea na Ukonga, Mhe. Agnesta Lambart Kaiza na Mhe. Bakari Shingo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here