Rais Dkt. Mwinyi: Serikali ya Awamu ya Nane kuendelea kuwekeza katika elimu bora na ujuzi kwa vijana

ZANZIBAR- Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali ya Awamu ya Nane itaendelea kuwekeza katika ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya skuli, pamoja na kuimarisha elimu ya ufundi na mafunzo ya amali ili wananchi wapate elimu bora na vijana wawe na ujuzi unaokidhi mahitaji ya soko la ajira na uchumi wa kisasa.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo Novemba 16, 2026 wakati akiweka mawe ya msingi ya ujenzi wa Skuli ya Msingi Mtopepo na karakana nne za kisasa za uhandisi katika Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia (KIST), Mkoa wa Mjini Magharibi.

Amesema, Serikali inaendelea kujenga skuli za kisasa zenye miundombinu bora, ikiwemo maabara na TEHAMA, huku skuli mpya ya Mtopepo ikiwa na ghorofa nne, madarasa 50 na lifti.
Aidha, karakana za KIST zitatoa mafunzo ya vitendo katika fani za Uhandisi wa Ujenzi, Uhandisi wa Mitambo, Useremala na Ufundi wa Magari, hatua itakayoongeza fursa za vijana kupata ujuzi na kujiandaa na soko la ajira.

Rais Dkt. Mwinyi amewataka wakandarasi kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kwa viwango vya ubora, huku akitoa shukrani kwa Taasisi ya Zayed na Ubalozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) nchini Tanzania kwa kushirikiana na Serikali katika kuimarisha sekta ya elimu Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here