Simba SC yapinga kauli za Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi TFF, yataka jibu rasmi

Na DIRAMAKINI 24 | Dar es Salaam

BODI ya Wakurugenzi ya Simba Sports Club imesikitishwa na kauli zilizotolewa hadharani na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuhusu Uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo.
Katika taarifa iliyotolewa kwa umma na hofu hiyo Novemba 15, 2026, Bodi hiyo imewataka wanachama, mashabiki, wapenzi, wadhamini na wadau wote kuwa watulivu, huku ikisisitiza kuwa Simba ni taasisi moja inayozungozwa na Katiba moja.

Barua ya Novemba 13 haijajibiwa

Bodi imesema kuwa, tarehe 13 Novemba 2026, iliandikia TFF barua rasmi ikieleza msimamo wake kuhusu uendeshaji wa mchakato wa uchaguzi, ikitoa mapendekezo ya kuuboresha na kuiomba shirikisho hilo kutoa uamuzi wa maandishi.

Hata hivyo, badala ya kujibu barua hiyo kwa njia rasmi, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi alijibu kupitia vyombo vya habari, jambo ambalo Bodi inaliona kuwa halikubaliki kwa chombo kinachosimamia mpira wa miguu nchini.

Kwa msingi huo, Simba imeiomba TFF kutoa majibu rasmi ya maandishi kwa barua yake.

Hakuna Simba mbili

Taarifa hiyo pia imekanusha vikali madai kuwa klabu hiyo ina pande mbili zinazopingana, pamoja na madai kuwa kuna ofisi mbili; moja ya Mwekezaji iliyopo Masaki na nyingine ya Mzee Mangungu iliyopo Msimbazi.

Bodi imesema kauli hizo si za kweli, zinachochea mgawanyiko miongoni mwa wadau na zina madhara ya kisheria kwa taswira ya taasisi.

Simba ni moja, Katiba ni moja

Kuhusu uongozi, Bodi imesisitiza kuwa Simba inaongozwa na Katiba moja, ambayo ni Toleo la 2018 lililofanyiwa marekebisho tarehe 30 Novemba 2025 na kusajiliwa rasmi tarehe 18 Februari 2026.

Kila mwanachama, shabiki, mdhamini, mchezaji, kocha na mfanyakazi wa klabu anatakiwa kutambua ukweli huo kwamba Simba ni moja.

Msimamo wa klabu kuhusu uchaguzi

Simba imesisitiza dhamira yake ya kuwa na uchaguzi huru, wa haki, wa wazi na unaoaminika, kwa mujibu wa Katiba yake, Kanuni zake za Uchaguzi, pamoja na kanuni za TFF na FIFA, katika mazingira ya kuheshimiana na kuelewana.

Aidha, jopo la wanasheria wa klabu linaendelea kutathmini hatua zaidi za kisheria dhidi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF.

Mwisho wa taarifa hiyo, Bodi imewaomba wanachama, mashabiki na washirika wote kuendelea kuwa watulivu na wamoja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here