NA DIRAMAKINI
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya mvua kubwa kwa siku ya leo Ijumaa, Novemba 13, 2026.
Hayo ni kwa mujibu wa utabiri wa hali ya hewa uliotolewa leo saa 9:30 mchana, ambao unahusu pia utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo kuanzia saa 3:00 usiku wa leo kwa Novemba 14, 2026.
Kwa mujibu wa TMA, tahadhari ya mvua kubwa imetolewa kwa maeneo machache ya mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara, Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Singida, Dodoma, Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa na Njombe.
Uwezekano wa mvua hiyo kutokea ni wastani, huku kiwango cha athari zinazoweza kutokea kikiwa kikubwa.
Athari inayoweza kujitokeza ni mafuriko kuathiri baadhi ya maeneo, na wananchi wameaswa kuchukua tahadhari.
Mbali na tahadhari hiyo, TMA imetoa angalizo la mvua kubwa kwa maeneo machache ya mikoa ya Kigoma, Tabora na Katavi. Katika mikoa hiyo, uwezekano wa kutokea ni wastani, na kiwango cha athari zinazoweza kutokea pia ni wastani.
Kwa utabiri wa saa 24 zijazo, mikoa ya Mara na Simiyu, Dodoma na Singida, pamoja na Manyara, Arusha na Kilimanjaro, inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu, mvua na ngurumo katika baadhi ya maeneo na vipindi vifupi vya jua.
Mkoa wa Morogoro, mikoa ya Kigoma, Tabora na Katavi, Kagera, Shinyanga, Mwanza na Geita, pamoja na Rukwa, Iringa, Njombe, Songwe na Mbeya, inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vifupi vya jua.
Visiwa vya Unguja na Pemba, Tanga na Dar es Salaam, Ruvuma, Mtwara na Lindi, pamoja na Mkoa wa Pwani ukijumuisha Visiwa vya Mafia, inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
TMA imeongeza kuwa vipindi vifupi vya mvua kubwa vinatarajiwa katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Mara, Simiyu, Morogoro, Dodoma, Singida na Tanga.
TMA imeongeza kuwa vipindi vifupi vya mvua kubwa vinatarajiwa katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Mara, Simiyu, Morogoro, Dodoma, Singida na Tanga.Kuhusu viwango vya joto kwa siku ya leo, Arusha inatarajiwa kuwa na joto la juu la nyuzi 27 na la chini la nyuzi 15, huku jua likiwa linachomoza saa 12:13 na kuchwa saa 12:24.
Dar es Salaam inatarajiwa kuwa na joto la juu la nyuzi 32 na la chini la nyuzi 21, jua likichomoza saa 11:57 na kuchwa saa 12:18.
Dodoma inatarajiwa kuwa na joto la juu la nyuzi 27 na la chini la nyuzi 17, jua likichomoza saa 12:12 na kuchwa saa 12:31.
Kigoma inatarajiwa kuwa na joto la juu la nyuzi 27 na la chini la nyuzi 20, jua likichomoza saa 12:37 na kuchwa saa 12:54.
Mbeya inatarajiwa kuwa na joto la juu la nyuzi 27 na la chini la nyuzi 15, jua likichomoza saa 12:17 na kuchwa saa 12:44.
Iringa inatarajiwa kuwa na joto la juu la nyuzi 25 na la chini la nyuzi 15, jua likichomoza saa 12:10 na kuchwa saa 12:33.
Njombe inatarajiwa kuwa na joto la juu la nyuzi 24 na la chini la nyuzi 12, jua likichomoza saa 12:09 na kuchwa saa 12:39.
Mwanza inatarajiwa kuwa na joto la juu la nyuzi 27 na la chini la nyuzi 19, jua likichomoza saa 12:28 na kuchwa saa 12:37.
Tabora inatarajiwa kuwa na joto la juu la nyuzi 28 na la chini la nyuzi 20, jua likichomoza saa 12:25 na kuchwa saa 12:42.
Tanga inatarajiwa kuwa na joto la juu la nyuzi 32 na la chini la nyuzi 23, jua likichomoza saa 12:00 na kuchwa saa 12:17.
Zanzibar inatarajiwa kuwa na joto la juu la nyuzi 31 na la chini la nyuzi 23, jua likichomoza saa 11:57 na kuchwa saa 12:18.
Kuhusu upepo wa Pwani, unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya kilomita 20 kwa saa kwa Pwani yote, kutoka Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Kaskazini Mashariki kwa Pwani ya Kusini. Hali ya bahari inatarajiwa kuwa na mawimbi madogo.

Kwa siku zinazofuata, Jumamosi, Novemba 14, 2026, angalizo la mvua kubwa limetolewa kwa maeneo machache ya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Singida, Dodoma, Morogoro, Tanga, Mara na Simiyu.
Uwezekano wa kutokea ni wastani, kiwango cha athari ni wastani, na athari inayoweza kujitokeza ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji. TMA imewataka wananchi kuzingatia na kujiandaa.
Jumapili, Novemba 15, 2026, hakuna tahadhari. Jumatatu, Novemba 16, 2026, hakuna tahadhari. Jumanne, Novemba 17, 2026, hakuna tahadhari.
