Mwinjilisti Temba aibua hoja Bandari Kavu ya Kwala (Vigwaza)

 NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Muhubiri na Mwinjilisti wa Kimataifa wa Kanisa la Penuel Healing Ministry la Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam, Alphonce Temba ameiomba Serikali isaidie kujua wafanyabiashara wanaohujumu kuanza kwa Bandari Kavu Vigwaza maana kila mipango ya serikali inapowekwa ili kuanza haifanikiwi.

Matokeo yake misongamano ya malori Dar es Salaam imekuwa tatizo sugu kuanzia Taifa, Buguruni, Ubungo hadi Kimara. Hasa jioni watu wanavyotoka makazini, mambo yote yametimia, mkandarasi wa barabara hajalipwa na kapunguza karibu wafanyakazi wote huku akiwa ametandika kifusi na kujenga madaraja njia nzima karibu kilomita 15 sasa nini kitatokea? Wakati wa masika udongo wote utasombwa na maji ya mvua na kisha kazi kuanza upya mara tatu ya gharama ya sasa, itabidi Mkandarasi alipwe.

Sasa sijajua hilo kwa Serikali inayokusanya kodi na tozo zote hizi ni sahihi kulipa tena huku vijijini maji, zahanati,barabara na kadhalika bado ni changamoto.

Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan tunakuomba uingilie kati kadhia hii, kuokoa mambo mengi kama nilivyoainisha hapo juu, huu pia ni msimu wa ligi umeanza uwanja wa taifa na mechi za kimataifa watu wa Kibaha, Mbezi,Bunju, hivyo shughuli ya kufika nyumbani ikijumuishwa na watu wanaotoka makazini jioni wako wanaofika mpaka saa tano ya usiku.

Tunaomba Bandari kavu Vigwaza ianze huku barabara ikijengwa mbona huko Congo DRC mfano kule Kolezi Lubumbashi ziko njia katika migodi hadi kilomita 100 hazina lami na magari toka Afrika Kusini, Botswana, Namibia Zimbabwe na Msumbiji yanabeba mizigo kupeleka katika migodi vivyo hivyo huko Sudani Kusini nako usiseme. Mwaka huu, 2021 hilo linawezekana kuanza.
Aliyekuwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mheshimiwa Izack Kamwele alitoa maagizo makubwa sana ya serikali ya nini kifanyike na muda wa kuhamia kwa shughuli zote za bandari kavu ikiwa ni pamoja na kupokea makontena kufanya minada na kuanza kushusha mizigo yote mwaka 2020.

Hata hivyo, aligusia ICD (Yadi) zote za jijini Dar es Salaam kutokuhifadhi tena mizigo na matokeo yake mizigo yote kupokelewa katika bandari kavu ya Kwala na kwa njia hiyo ilikuwa ikipuguza sana misongamano mkubwa wa malori jijini Dar es Salaam ambao unasababisha karibu kila siku za kazi kupotezwa kwa zaidi ya bilioni tatu kutokana na kadhia hiyo, kama vile watanzania wengi wanavyolalamika kuwa, mambo mazuri mengine ya Serikali uhujumiwa na baadhi ya watanzania wafanyabiashara waliowekeza katika baadhi ya miradi, ndiyo mfano tunaoona ni huu wa yadi zilizopo mjini zinazomilikiwa na matajiri ambazo wamekuwa wakizikodi kwa mwezi kuanzia dola 4000 na kuendelea.

Wamekuwa wakihofia kuwa endapo serikali itaanzisha bandari Kwala itasababisha shughuli zao kufa, hivyo kuhusika kutumia baadhi ya watendaji wachache wa serikali kudhohofisha uharakishwaji wa maamuzi ya kuanza kwa michakato kadha wa kadha ambayo ingefanikisha malengo na nafuu kubwa kwa jamii. 

Hivyo suala hili la Bandari kavu Kwala endapo Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan hataingilia kati litakuwa likipigwa danadana na kuendelea kudhohofisha uchumi wa Tanzania, unaoanza kukua kutokana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Sita ambayo imeweka mkazo mkubwa kuitangaza nchi na kuanzisha viwanda vya kimkakati hili kuokoa mamilioni ya ajira ya vijana wetu wanaomaliza shahada mbalimbali kila kukicha.

Jambo lingine napenda kuishauri serikali kwa kuwa ineazimia kubadilisha mkoa wa Pwani kuwa mkoa wa viwanda na kutenga maeneo kadhaa ya viwanda ambapo ujenzi mkubwa unaendelea kwa kasi sana ni matumaini yangu serikali ya CCM, kweli imedhamiria kufufua uchumi na kutokomeza kabisa tatizo la ajira kwa asilimia kubwa hila pamoja na kuwa ujenzi huo unaendelea maeneo ya Kibaha mjini Lulanzi, Zegereni,Mlandizi Disinyala na Vigwaza kambini ktk shamba la Narco bado serikali inatakiwa kuwa na njia mpya za kimkakati na si kutegemewa kwa njia moja tu ya Morogoro Road hivyo basi ipo njia ambayo inaanzaia Kibaha Maili moja kupitia hospitali ya Tumbi kupita Boko, Soga, Kibwemwenda, Changombe hadi njia panda ya Mzenga kupanda hadi Ruvu station hadi Bandari kavu Kwala.

Kwenda moja kwa moja hadi Magindu ,Chaua na kutokea Chalinze au kuja Zegereni hadi Mlandizi njia hiyo ambayo bado ipo serikali inapaswa kuiandaa kwa ajili ya vizazi vijavyo na sasa TANROADS iweze kuipa hadhi na kuiwekea mawe kabla wananchi hawajajenga kiholela.

Ikumbukwe Tanzania miaka hamsini ijayo itakuwa na wananchi zaid ya milioni mia moja. 

Hivyo lazima leo kuwe na mipango ya kusaidia kizazi kijacho kwa kutenga barabara zitakazowasaidia kama vile kipindi cha mkoloni walivyokuwa wametenga barabara ya Morogoro road kuanzia Ubungo mpaka Kibaha. 

Kufunguliwa viwanda Mkoa wa Pwani kuenende na ufunguliwaji wa njia nyingi zaidi hili kukwepa misongamano isiyo rasmi huko baadaye. 

Mweshiwa Rais nakuomba uwe mkali sana katika haya niliyoyashauri nakumbuka mwaka 2008 nilivyoshauri Serikali ya Awamu ya Nne kuhamisha mzani wa magari Kibaha kuhamia Vigwaza, wengi walinipinga na ndipo nilipomwandikia barua Waziri Mkuu wakati huo, Mheshimiwa Mizengo Pinda akakubaliana na ushari wangu na kupeleka mswada Bungeni na leo hii tunaona faida zake ni imani ushauri wangu utafanyiwa kazi kwa lengo la kuipata Tanzania iliyo bora zaidi.

Post a Comment

0 Comments