HASHIM Rungwe na Mgombea Mwenza (CHAUMA), Mohammed Masoud leo wameidhinishwa na Tume ya Taifa Uchaguzi ( NEC) kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Oktoba 28, mwaka huu.
Rungwe ambaye amekuwa akisisitiza kuwa, akichaguliwa lazima aipeleke bahari Dodoma na wanafunzi kula ubwabwa wa kushiba anakuwa mgombea wa 12 kuidhinishwa na tume chini ya Mwenyekiti wake, Jaji mstaafu Kaijage.
Wengine ambao tayari wameidhinishwa ni Dkt. John Magufuli (CCM), John Shibuda (ADA Tadea), Leopard Mahona (NRA), Queen Sendiga (ADC),Profesa Ibrahim Lipumba (CUF), Mutamegwa Mugaiwa (SAU), Cesilia Mwanga (Demokrasia Makini), Bernard Membe (ACT Wazalendo), Twalib Kadege (UPDP), Philip Fumbo (DP), Yeremia Maganja (NCCR Mageuzi).
Kwa habari au matangazo (diramakini@gmail.com)
www.diramakini.co.tz
