RAIS MAGUFULI AWASILISHA FEDHA ZA MICHANGO ILIYOTOLEWA KATIKA HARAMBEE YA KUCHANGIA UJENZI WA MSIKITI WA CHAMWINO, DODOMA

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli leo amewasilisha fedha za michango iliyotolewa katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Msikiti wa Chamwino mkoani Dodoma.

Fedha hizo  zimewasilishwa na Katibu wa Rais, Ngusa Samike kwa Sheikh Mkuu wa Wilaya,Suleiman Abdallah Matitu muda mfupi baada ya swala ya Adhuhuri iliyofanyika katika Msikiti uliopo hivi sasa.

Pamoja na kukabidhi fedha hizo,Rais Magufuli amewapongeza na kuwashukuru watu wote waliounga mkono na wanaoendelea kuunga mkono uchangiaji wa ujenzi wa Msikiti mpya na wa kisasa wa Wilaya ya
Chamwino.

Rais Magufuli amesema, Msikiti huo utajengwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), na ujenzi wake utaanza wiki hii.

Amesema,watu mbalimbali wameguswa bila kujali madhehebu ya dini waliyonayo na kwamba hiyo ni udhibitisho wa umoja na mshikamano
walionao Watanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

1 Comments

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here