RC Kunenge aipongeza Jumuiya ya Khoja Shia kupitia programu yake ya “Husayni Blood Drive” kwa kufanikisha zoezi la uchangiaji damu kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Damu Salama na Hospitali ya Ebrahim Haji

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge ameipongeza Jumuiya ya Khoja Shia kupitia programu yake ya “Husayni Blood Drive” kwa kufanikisha zoezi la uchangiaji damu kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Damu Salama na Hospitali ya Ebrahim Haji. 

Zoezi hilo la uchangiaji damu limefanyika jana katika Hospitali ya Ebrahim Haji iliyopo jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha kumbumbuku ya kifo cha mjukuu wa Mtume Muhammed (SAWW), Imam Hussain.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge (katikati) akipokea maelezo kutoka kwa mmoja wa viongozi wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithnasheri, Dkt. Shaneabbas Jaffer    wakati wa zoezi la uchangiaji damu lililofanyika katika Hospitali ya Ebrahim Haji kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Damu Salama.

Pia ikiwa ni kuendeleza utamaduni wa kujitolea kwa jamii ambao ni msingi mkuu wa ujumbe wa Imam Hussain. 

Katika zoezi hilo, Mkuu wa Mkoa amepongeza jumuiya ya Khoja Shia Ithnasheri kwa tukio hilo lenye upendo kwa kuwa linaenda kuokoa maisha ya watu.

 “Nimeambiwa kuwa zoezi hili limefanyika kwa zaidi ya miaka 15 na kukusanya zaidi ya lita 5000 za damu ambazo zimesaidia kuokoa maisha ya watanzania wengi jambo ambalo ni lenye upendo mwingi kwani watu hawa wanachangia damu bila kujali inakwenda kumsaidia nani,"alisema Mkuu wa Mkoa.

Mkuu wa Mkoa alisema, watu wengi wanapenda kutoa msaada pale ambapo wana uhakika wa kupata shukrani na hivyo kutoa msaada kwa watu wanaowajua au kuwaona, lakini Jumuiya ya Khoja Shia Ithnasheri imefanya sadaka iliyob kwa kutoa damu kwa watu wasiowajua ambao hawatapata hata nafasi ya kuwashukuru na hiyo ndiyo sadaka bora kwa mujibu wa vitabu vya dini. 

RC Kunenge alitumia fursa hiyo kumpongeza Mwenyekiti wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithnasheri, Azim Dewji kwa kushiriki katika matukio mengi ya kitaifa ikiwemo kutoa nyumba yake binafsi ili kutumika kama kituo cha kuhudumia wagonjwa waliopata maambukizi ya Corona.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithnasheri, Azim Dewji alisema kuwa, jumuiya hiyo imekuwa ikishiriki katika mambo mengi ya kijamii ambapo mapema mwaka huu, jumuiya hiyo hiyo ilitumia siku 45 kujenga wodi mpya yenye vitanda 60 katika Hospitali ya Ebrahim Haji ili kusaidia wagonjwa waliopata maambuzi ya Corona. 

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithnasheri, Azim Dewji akitoa maelezo wakati wa zoezi la uchangiaji damu lililoendeshwa na Jumuiya ya Khoja Shia Ithnasheri kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Damu Salama na Hospitali ya Ebrahim Haji jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo kutokana na kupungua kwa maambukizi ya Corona nchini, wodi hiyo sasa itatumika kuhudumia akina mama na watoto. 

Pamoja na hilo kila Jumamosi hospitali hiyo hutoa huduma bure za matibabu kwa watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu ikiwa ni sehemu ya mchango wake kwa jamii.

Nae Mkuu wa Idara ya Ukusanyaji Damu Kanda ya Mashariki, Judith Goshashy ameipongeza Jumuiya ya Khoja Shia Ithnasheri kwa kuwa wachangiaji wazuri wa damu kwa Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS) tangu walipoanza kushirikiana nao mnamo mwaka 2008. 

“Katika kipindi cha miaka 5 iliyopita tumekuwa tukipokea wastani wa wachangiaji damu 440 kila mwaka kutoka katika jumuiya hii, jambo ambalo ni la kupongezwa sana ukizingatia huwa wanajitolea damu mara mbili kwa mwaka,"alisema Judith.  

Sheikh Sayed Idairous ambaye ni mmoja wa viongozi wa dini kutoka katika Jumuiya ya Khoja Shia Ithnasheri, alisema kuwa, wajibu wa viongozi wa dini katika nchi ni kujenga undugu bila kujali itikadi za dini wala kabila na hivyo wao wamechagua kufanya zoezi hilo la uchangiaji damu ambalo linakwenda kusaidia watu bila kujali itikadi zao. 

Sheikh Sayed Idairous kutoka katika Jumuiya ya Khoja Shia Ithnasheri akitoa maelezo wakati wa zoezi la uchangiaji damu lililoendeshwa na Jumuiya ya Khoja Shia Ithnasheri kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Damu Salama na Hospitali ya Ebrahim Haji jijini Dar es Salaam.

“Damu hii inayotolewa hapa haitouliza dini ya mtu wala kabila lake bali itakwenda kusaidia kukoa maisha ya watu na huo ndio wajibu wetu ,"alisem Sayed.

Pamoja na zoezi la kuchangia damu,Jumuiya ya Khoja Shia Ithnasheri pia hushiriki katika shughuli nyingine za kijamii ikiwemo utoaji wa maji safi, uchunguzi na upasuaji wa mtoto wa jicho, uchunguzi wa saratani zinazoathiri wanawake ikiwemo saratani ya matiti na mlango wa kizazi. “Huduma hizi zimekua zikifanyika kwa takribani miaka mitano sasa na hutolewa bila malipo kwa wagonjwa wote wanaojitokeza,”alisema Dkt.Alihussein Molloo ambae ni mwanajumuiya ya Khoja Shia Ithnasheri na Mkurugenzi wa Hospitali ya Ebrahim Haji.



.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here