TAASISI YA MOYO (JKCI) YAPOKEA MASHINE YA KUPIMA UMEME WA MOYO

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI),Prof. Mohamed Janabi akimpulizia kisafisha mikono (hand sanitizer ) Daktari bingwa wa magonjwa ya watoto Antke Zuechner wa Jamii ya Ujerumani kwa magonjwa ya watoto ya Ukanda (Germany Society for tropical pediatrics) mara baada ya kumkabidhi msaada wa mashine ya kupima umeme wa moyo (Electrocardiogram) kwa watoto wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. Thamani ya mashine hiyo ni milioni 17.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimshukuru Daktari bingwa wa magonjwa ya watoto Antke Zuechner wa Jamii ya Ujerumani kwa magonjwa ya watoto ya Ukanda (Germany Society for tropical pediatrics) kwa msaada wa mashine ya kupima umeme wa moyo (Electrocardiogram) kwa watoto wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha magonjwa ya moyo kwa watoto Dkt. Sulende Khuboja akifuatiwa na Mkuu wa kitengo cha Mafunzo na Utafiti Dkt. Naiz Majani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza na wazazi kuhusu umuhimu wa kufanya kipimo cha kuchunguza moyo wa mtoto aliyepo tumboni kwa wamama wajawazito (Fetal Cardiograph). Wazazi hao walifika katika Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuwaleta watoto wanaotibiwa Jkci kliniki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwaeleza madhara ya mafuta mwilini wagonjwa waliokuwa wanasubiri kufanyiwa vipimo vya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiogram – ECHO) na Umeme wa moyo (Electrocardiogram – ECG) wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. Picha na JKCI

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) yapokea msaada wa mashine ya kupima umeme wa moyo (Electrocardiogram) yenye thamani ya shilingi milioni 17 kutoka kwa Jamii ya Ujerumani kwa magonjwa ya watoto ya Ukanda (Germany Society for tropical pediatrics) ambayo itatumika kwa ajili ya watoto wanaotibiwa katika Taasisi hiyo

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here