Namungo FC, Biashara United wachezesha karata vizuri michuano Ligi Kuu Bara

MSIMU mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara umeanza kwa timu za Biashara United kutoka mkoani mara na Namungo FC ya mkoani Lindi kufanya vizuri.
Ni baada ya ushindi wa 1-0 zote dhidi ya Coastal Union ya Tanga na Gwambina FC ya Mwanza ambapo katika Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi bao pekee la Bigirimana Blaise dakika ya 64 liliwapa wenyeji,Namungo FC ushindi wa 1-0.

Aidha, katika Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara bao pekee Kelvin Friday katika dakika ya 88 limewapa ushindi wa 1-0 timu ya Biashara United.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news