DODOMA-Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano inatekeleza Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi ambayo inalenga kuwawezesha vijana wa Kitanzania kupata ujuzi wa stadi za kazi stahiki ili kuweza kushindana katika soko la ajira.
Katika kutekeleza programu hii, Ofisi imeingia makubaliano na vyuo 46 vinavyotoa mafunzo ya ufundi stadi yaliyoidhinishwa na Serikali.
Mafunzo haya yanatolewa katika fani mbalimbali zikiwemo:Urembo na Ususi, Ushonaji nguo na ubunifu wa mitindo, Ufundi bomba, Uashi,Fundi magari, Ujenzi, Useremala, Uungaji vyuma, Uchomeleaji, Upakaji rangi, Maandishi ya alama, Upishi,Utengenezaji wa vipuri vya mitambo,Umeme wa majumbani na viwandani,Umeme wa magari, Umeme wa jua (solar),Huduma za hoteli na utalii, Ukataji madini,Ufundi vyuma na fani nyingine zinazohusiana.
Serikali itagharamia ada za mafunzo kwa asilimia 100. Mwanafunzi/Mzazi/Mlezi atawajibika kugharamia gharama nyingine kama nauli ya kwenda na kurudi chuo.Mafunzo yatadumu hadi tarehe 26 Januari 2026.
Waombaji wanatakiwa kuchukua fomu katika Vituo vya Ufundi Stadi (VETA) vya Mikoa na Wilaya vilivyopitishwa na Serikali ambavyo vimeorodheshwa hapa chini;
Tags
Ajira kwa Vijana
Breaking News
Fursa za Mafunzo
Habari
Matangazo
Tangazo
Vijana Tanzania
Wizara ya Kazi na Ajira







