Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Biswalo Mganga amesema, yeyote mwenye mwenye lengo la kuvuruga amani ya nchi atashughulikiwa bila kujali cheo, jinsia wala dini katika kipindi cha uchaguzi na hata baada ya uchaguzi, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Amesema hayo wakati akizindua Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wilayani Mufindi iliyopo Mjini Mafinga Mkoa wa Iringa ambapo amesisitiza kuwa, jukumu la kulinda amani ya nchi ni jukumu la kila Mtanzania.
DPP amesema, kila mwananchi ana wajibu wa kufuata sheria na taratibu za nchi ili kuepuka vurugu zinazoweza kusababisha uvunjifu wa amani nchini.
Amesema kuwa, nchi nyingi ambazo hazina amani waathirika wakubwa wamekuwa watoto na wanawake, hivyo jamii inatakiwa kuona wajibu wa kila mmoja kuwa mlinzi wa amani na usalama wa nchi.
Pia amesema kuwa, ofisi yoyoe inayohusika na usalama duniani kote ina jukumu la kuhakikisha inalinda amani ya nchi husika pamoja na kuhakikisha watu wake wanafuata sheria na taratibu za nchi, hivyo wananchi wanaombwa kutoa ushirikiano kwa ofisi hiyo ili ulinzi, usalama na amani viendelee kutawala nchini muda wowote.

Amesema kuwa, lengo la ofisi hiyo kufunguliwa wilayani Mufindi ni kuhakikisha wanaondoa malalamiko ya kutotendewa haki wananchi wanapokuwa na kesi na kusogeza huduma hiyo karibu.
DPP amesema, awali watu walikuwa wanafuata huduma hiyo mkoani Mbeya na baadae ofisi ya mkoa ilifunguliwa mkoani Iringa ambapo watu wa Mufindi bado walikuwa wanatumia muda mwingi kuzifuata huduma hizo na ofisi hizo.
Amewaomba wakuu wa wilaya zote hapa nchini kuiga mfano wa Wilaya ya Mufindi waliotoa majengo yao bure kwa ajili ya kufungua Ofisi ya Mashtaka na kufanya idadi za ofisi hiyo kufikia 15 katika wilaya 139 Tanzania nzima jambo ambalo limekuwa likichelewesha usikilizaji wa mashtaka yanapowafikia.
Amesema kuwa,ili kupata amani na haki kila mmoja anatakiwa kuona jukumu alilonalo ni la kuwa mlinzi wa kulinda usalama wa taifa badala ya kugeuka kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani hivyo kila mtu anawajibu wa kufuata sheria na taratibu za nchi zilizowekwa.
DPP Maganga amesema, sheria haichagui mtu kwani ikivunjwa na yeyote iwe kiongozi wa dini ama mwanansiasa ofisi yake haitasita kuwachukulia hatua mara moja.
Mkuu wa Wilaya Mufindi, Jamhuri David amesema kuwa, wakazi wa Wilaya ya Mufindi walikuwa wanaifuata haki Mkoa wa Iringa jambo ambalo lilikuwa linawalazimu kutumia muda mrefu hasa kwa wana Mufindi ambao wengi wao ni wafanyabiasha, amewataka kutumia ofisi hiyo kupata haki.
DC huyo amesema kuwa, wananchi wanapoitumia ofisi hiyo watapata fursa ya kupata elimu ya namna ya kupata haki ambayo itawasaidia kuondokana na dhana ya upendeleo au kubambikizwa kesi kwa baadhi ya watu wilayani humo.

Tags
Habari