Magazeti leo Juni 23,2026

Meneja wa kampasi ya Dodoma ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Prof. Epaphra Manamba amesema katika kuendana na mahitaji ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 IAA itaendelea kuwekeza katika mitaala itakayojikita kwenye elimu – ujuzi (Competence based ) na ubunifu ili kuwaandaa wataalam watakaokuwa na uwajibikaji jumuishi katika kujenga Uchumi Jumuishi.
Prof. Manamba ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika banda la IAA kwenye Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.

“Dira ya Taifa ya 2050 imeipa sekta binafsi nafasi kubwa, tunapoongelea uwajibikaji jumuishi na uchumi jumuishi sekta binafsi inahusika kwa asilimia 100;sekta binafsi imepewa nguvu kwa sababu maendeleo ya nchi hii yatachangiwa na sekta binafsi na serikali itaandaa miundombinu ili kuiwezesha sekta binafsi kufanya kazi yake.”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here