Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, amekamilisha haki yake ya kikatiba kwa kupiga kura katika eneo la Kilimani, jijini Dodoma.
Katika
eneo hilo ambapo pia awali na baadaye walionekana viongozi wengine
mbalimbali wa Serikali, chama na taasisi binafsi, Dkt. Abbasi alikaa
kwenye foleni kama kawaida na wananchi wengine na alipomaliza kupiga
kura akasisitiza:
"Nimekamilisha haki yangu ya
kikatiba kwa furaha sana kwa sababu tukiwa pale kwenye foleni tunapiga
stori za hapa na pale wananchi walikuwa wanasema sio wote tuliopiga nao
kura mwaka 2015 leo wamepata bahati tena kama hii kwa maana ya uhai
kushiriki nasi. Hivyo ni jambo si tu la kikatiba lakini lenye hisia
kubwa kibinadamu na kiroho mtu anapolitimiza."
Dkt.
Abbasi alieleza kuridhishwa na hali ya utulivu kituoni hapo na
kusisitiza ambao hawajakamilisha haki yao wajitokeze kuwahi kabla ya
muda uliowekwa na Tume kukamilika.
"Kituoni
kwetu hapa na kwingine nilikopita hapa Dodoma hali ni shwari. Tume
imejipanga hasa utaratibu ni mzuri na wa uhakika kwani kila hatua
unaelekezwa wasimamizi na makarani wa uchaguzi na mawakala wa vyama
wanajiridhisha kwa kila jina linalotajwa.
"Ukiacha
kelele za baadhi ya wanasiasa wachache Watanzania wengi wameitikia wito
wa amani na wengi tuliopiga nao kura hapa kila mmoja anasema anarejea
nyumbani au kwenye shughuli zake kwa ajili ya kuendelea na masuala
mengine atasubiri matokeo kuanzia jioni," alisema Dkt. Abbasi.
Tags
Habari
