Bandari ya Dar es Salaam yaongoza kwa ubora barani Afrika

Baada ya Hifadhi ya Taifa Serengeti kushinda tuzo ya kuwa Hifadhi Bora katika Bara la Afrika kwa mwaka 2020 nayo Bandari ya Dar es Salaam imeibuka kuwa bandari inayoongoza kwa ubora barani Afrika, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Tuzo hiyo ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti imetangazwa Novemba 9,2020 na Taasisi ya World Travel Awards (WTA) ya nchini Marekani kwa njia ya mtandao.
Muonekano wa kisasa wa Bandari ya Dar es Salaam.
 
Hiyo ikiwa ni mara ya pili kwa Hifadhi ya Taifa Serengeti kushinda katika Kundi la Hifadhi zinazoongoza kwa ubora zaidi Bara la Afrika baada kushinda pia mwaka 2019.

Aidha kwa upande wa bandari, Taasisi ya World Travel Award (WTA) ya London, Uingereza, Jumanne ya wiki hii imeipigia kura Bandari ya Dar es Salaam kuwa Bandari inayoongoza kwa meli za utalii na ubora wa huduma barani Afrika.

Mafanikio haya kwa Bandari ya Tanzania ni ya kwanza kwa bandari kubwa zaidi nchini kupata tuzo katika kipengele cha crème de la crème kilichojumuisha bandari nyingine kama Bandari za Elizabeth, Cape Town na Durban zote za Afrika Kusini, Bandari ya Mobasa, Kenya na Bandari ya Zanzibar.

Mwandishi Diramakini anaendelea kukusanyia data zaidi kwa ajili ya kukujuza kuhusiana na rasilimali za Tanzania zilivyo na matokeo chanya ndani na nje ya Tanzania, hivyo endelea kufuatilia hapa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news