Haaland awapa shangwe mashabiki wa Borussia Dortmund

Mnorway Erling Haaland (20) akishangilia baada ya kuifungia Borussia Dortmund mabao manne dakika za 47, 49, 62 na 79 katika ushindi wa 5-2 dhidi ya wenyeji, Hertha Berlin kwenye mchezo wa Bundesliga jana.

Kabumbu hilo safi lilitandazwa katika Uwanja wa Olympia mjini Berlin. Bao lingine la Borussia Dortmund lilifungwa na Raphael Guerreiro dakika ya 70, wakati ya Hertha Berlin yalifungwa na Matheus Cunha dakika ya 33 na Matheus Cunha kwa penalti dakika ya 79.

Post a Comment

0 Comments