Mdee afunguka mazito baada ya kuapishwa Mbunge Viti Maalum

Leo Novemba 24,2020 Mbunge wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Bi. Halima Mdee amewaahidi wanachama wa chama hicho kuwa wanakwenda bungeni kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu mkubwa, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Mdee ameyasema hayo katika viwanja vya Bunge leo muda mfupi baada ya kula kiapo pamoja na wabunge wenzake 18.

Mbunge huyo ambaye awali alikuwa Mbunge wa Kawe na ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA) amemshukuru Mheshimiwa Spika, Job Ndugai kwa kusimamia kiapo chao.

"Mheshimiwa Spika nikushukuru kwa kiapo kufanyika na kukamilika, nikishukuru chama changu kupitia wao sisi tumepata nafasi hii ya kukiwakilisha chama chetu. Viti hivi sio hisani ni sehemu ndogo ya ushindi mkubwa ambao chama chetu kilipata.

"Nikuhakikishie Mheshimiwa Spika tutafanya kazi kwa uaminifu kama kambi rasmi ya upinzani bungeni na kwa uadilifu mkubwa kwa viwango vilevile tulivyokuwa tunavifanya. Kuna vijana wapya sisi kama dada zao tunakuhakikishia watafanya kazi bora. Niwahakikishie wana CHADEMA tutafanya kazi mliyotutuma kwa uaminifu na uadilifu mkubwa sana.

Post a Comment

1 Comments