Serikali ya Awamu ya Nane kutoa elimu bora bila ubaguzi Zanzibar

Mkurugenzi wa Utumishi na Uendeshaji wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Bw.Omar Ali Omar (Bhai) amesema Serikali ya Awamu ya Nane chini ya uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi itahakikisha elimu inatolewa bila ya ubaguzi ili kuweza kuibua vipaji mbalimbali kwa wanafunzi hapa nchini.
Akizungumza katika mahafali ya Skuli ya Lion King Junior Academy katika ukumbi wa Taasisi Vuga mjini Unguja amesema elimu ni haki ya kila mwananchi bila kujali kuwa inatolewa kwa Skuli za binafsi au Serikali.

Aidha, amewashukuru walimu kwa jitihada kubwa walizoonesha kwani wameweza kuongeza idadi ya ufaulu na kufanikiwa kuibua vipaji mbalimbali katika skuli yao.
 
Amewataka wazazi kutenga siku maalum kwenda Skuli ili kuskiliza maendeleo ya watoto wao kwani kufanya hivyo kutawasaidia kuweza kujua maendeleo na mahudhurio ya watoto wao.

Pia mkurugenzi ameupongeza uongozi wa skuli kwa kuwa karibu na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kwa kuhakikisha wanapata kibali cha kutoa elimu na kuzitaka skuli nyingine ambazo hazijapatatiwa usajili kufanya haraka kusajili ili kuepusha matatizo yasio ya lazima.
 
Amesema,elimu ni zawadi yenye thamani kubwa hivyo amewataka wazee wawekeze eLimu kupitia watoto wao kwani litakuwa ni jambo la busara kwa maisha ya watoto wao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Skuli ya Lion King Junior Academy, Majmoud Ibrahim Musallam amewataka wazazi na walezi kuwahamasisha watoto kuwapenda walimu na kuwathamini walimu wao kwani kufanya hivyo kutawasaidia wanafunzi kujenga mahusiano mazuri na walimu wao.

Aidha, amewataka wazazi kuacha tabia ya kuwasema vibaya walimu mbele ya watoto wao,kwani kufanya hivyo ni kumshushia hadhi mwalimu.
 
Amewasihi wanafunzi kuwapenda walimu wao na kuwataka kutokuwa na tabia ya kuwavunjia heshima walimu wao, kwani kufanya hivyo ni kuivunjia hadhi elimu watakayokuja kuitumia baadae.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news