Yanga SC kuja kivingine

Klabu ya Yanga ambayo ipo kileleni mwa Msimamo wa Ligi baada ya kufikisha alama 28 na kuwashusha Azam FC kwenye nafasi ya pili wakiwaa na alama zao 25, ipo katika mpango kabambe wa kuja kivingine, Mwandishi Diramakini amedokezwa.

Aidha, mbali na kukaa kwenye kilele cha msimamo wa Ligi Kuu, Yanga SC ni wababe wa Azam kwani katika mechi 25 walizokutana wameshinda mechi tisa dhidi ya nane za Azam FC huku wakitoka sare kwenye mechi nane.

Yanga pia wameendelea kuweka rekodi bora msimu huu kwani hadi sasa zikiwa zimeshachezwa mechi 12, ni timu pekee ambayo haijapoteza mchezo wowote wakipata sare katika mechi nne na kushinda mechi nane.

Moja ya chanzo kimeidokeza Diramakini kuwa, viongozi wa timu hiyo wamekuwa wakiumiza vichwa usiku na mchana ili kuhakikisha wanaifanya klabu hiyo kwenda mbele zaidi.

Wajumbe katika picha ya pamoja baada ya kikao cha kupitia ripoti ya mapendekezo ya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa Klabu ya Yanga yanayofanyika katika makao makuu ya La Liga mjini Madrid nchini Hispania. 

Kikao hicho kimehudhuriwa na Mhandisi Hersi Said kutoka Yanga, Marco De Santis Meneja Miradi wa LaLiga Afrika, Juan Botella Meneja wa LaLiga Afrika na Alvaro Paya Mwanamsafara wa LaLiga Tanzania na Rwanda.

Post a Comment

0 Comments