Koplo Minja azidi kuwa shujaa kwa uokozi wa watoto chooni

Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Kagera, Koplo Denis Minja aliyemuokoa Mtoto kwenye shimo la choo mwezi Mei, mwaka 2020 mjini Ngara Mkoa wa Kagera ameongoza tena wenzake kumuokoa mtoto wa miaka miwili Karagwe mkoani aliyetumbukia chooni. 

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Kagera, Inspekta Shaban Hamis Dawa amesema mtoto huyo alitumbukia kwenye shimo hilo wakati akimfuata mama yake.

Minja awali alimuokoa mtoto eneo la Murugwanza wilayani Ngara kwenye shimo la choo na Desemba 28, 2020 amemuokoa mtoto mwingine, Anekius Evarist (2) huko Kata ya Kayanga iliyopo Tarafa ya Bugene wilayani Karagwe mkoani hapa. 

Post a Comment

0 Comments