DC CHONGOLO APOKEA RIPOTI YA CHANGAMOTO YA TOPE KUTOKA KWA WATAALAMU WA JIOLOJIA

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo amepokea ripoti ya utafiti iliyofanywa na wataalamu wa Jiolojia kuhusiana na kuwepo kwa changamoto ya Tope katika eneo la Kunduchi jijini Dar es Salaam Novemba mwaka jana, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo akipokea taarifa ya Changamoto ya tope iliyotokea Kunduchi jijini Dar es Salaam kutoka kwa Mhadhiri wa Jiolojia wa Chuo Kikuu ch Dar es Salaam, Dk. Remigius Gama.

Mhe. Chongolo ampokea taarifa hiyo leo ofisini kwake kutoka kwa Timu ya wataalamu iliyokuwa inacunguza changamoto hiyo ikiongozwa na Mhadhiri wa Jiolojia kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam Dk. Remigius Gamba, ambaye ndio kiongozi mkuu wa kamati hiyo.

Akizungumza mara baada ya kupokea kwa taarifa hiyo, Mhe. Chongolo ameeleza kuwa mara baada ya kutokea kwa changamoto hiyo, Serikali ilichukua hatua ya kuunda kamati ya wataalamu kwa ajili ya kuchunguza hali hiyo na hivyo kuipongeza kutokana na kazi kubwa waliyoifanya.
Wajumbe wa kamati pamoja na watalamu waliohusika katika utafiti wa changamoto ya Tope iliyotokea Kunduchi Jijini Dar es Salaam Novemba mwaka jana.

Mhe. Chongolo ametaja watalamu waliohusika katika utafiti wa changamoto hiyo kuwa ni kutoka Taasisi ya Jiolojia na utafiti wa madini Tanzania (AGST), Chuo kikuu cha Dar es Salaam kupitia shule ya migodi na madini idara ya Jiosayansi, Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) pamoja na Chuo cha mafunzo ya Jiosayansi (AMGC).

Ameongeza kuwa kupitia ripoti hiyo, ushauri uliotolewa na wataalamu hao utafayiwa kazi kwa pamoja kama Serikali kuanzia ngazi ya wilaya hadi ile ya juu inayohusiana na uchakataji wa taarifa pamoja na utekelezaji wake.
Kaimu Mkurugenzi wa huduma za Jiolojia kutoka Taasisi ya Jiolojia na utafiti wa madini Tanzania bwana Maruvuko Msechu akiwasilisha Taarifa ya ripoti ya changamoto ya Tope iliyotokea Kunduchi Jijini Dar es Salaam Novemba mwaka jana.

Hata hivyo Mhe.Chongolo amesema kuwa utafiti huo ulikuwa ukifanyika kwa kushirkiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Abuubakari Kunenge na kwamba kutokana na umuhimu huo ataiwasilisha kwakwe ili aweze kujua matokeo ya kamati hiyo.

Hata hivyo Mhe. Chongolo amewataka wananchi kuacha kusikiliza taarifa zisizo rasmi kutoka katika vyanzo mbalimbali na badala yake wasikilize na kufuata maelekezo yatakayotolewa na Serikali kupitia watalaamu wake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news