Mfaransa Didier Gomes Da Rosa ndiye kocha mkuu wa Simba SC


Mtendaji Mkuu wa Simba SC, Barbara Gonzalez akimkabadhi jezi Kocha Mkuu mpya, Mfaransa Didier Gomes Da Rosa baada ya kusaini mkataba katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Awali klabu ya Simba imemtambulisha Mbrazil, Milton Nienov Huyu kuwa kocha wake mpya wa makipa, akichukua nafasi ya Muharami Mohammed 'Shilton' aliyeondolewa mwishoni mwa mwaka jana.

"Huyu ndio baba yetu katika milingoti mitatu ya Mabingwa wa nchi. Ndie mwenye jukumu la kuhakikisha makipa wetu wanakuwa bora maradufu," imesema taarifa ya Simba SC leo.

Milton Nienov amewahi kuwa kocha wa makipa wa klabu za Polokwane City, Lamontville Golden Arrows FC, Super Eagles FC, Free State Stars FC za Afrika Kusini na Club de Regatas Vasco da Gama, Sport Club Recifie na Figueirense FC za kwao, Brazil.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news