Uzinduzi wa bomba la mafuta mwezi ujao, kupisha maombolezo kifo cha Hayati Dkt.Magufuli

Hafla ya uzinduzi wa mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) iliyopangwa kufanyika karibuni imehairishwa, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI.

Uamuzi huo umefikiwa na Serikali ya Jamhuri ya Uganda ili kuomboleza kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kutokana na mchango mkubwa alioutoa katika mradi huo.

Serikali ya Uganda kupitia Mamlaka ya Petroli nchini humo (PAU) imetoa taarifa ikisema uzinduzi huo umeahirishwa hadi mwezi ujao.

PAU imesema uongozi mahiri wa Rais Magufuli uliweka msingi thabiti kwa mradi huo, ikiwemo makubaliano kati ya Uganda na Tanzania mwaka 2017 na mwaka jana.
Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki ni bomba la mafuta yanayosafirishwa nje nchi lenye urefu wa kilometa 1,445 ambalo litafirisha mafuta ghafi ya Uganda kutoka Kabaale – Hoima nchini Uganda kwenda kwenye peninsula ya Chongoleani karibu na bandari ya Tanga nchini Tanzania.Kwa nini njia hii imechaguliwa?

Kufuatia utafiti wa kina uliofanywa na serikali za Uganda, Tanzania na Kenya. Serikali ya Uganda ilichagua njia ya Kabaale (Hoima) – Tanga kwa sababu ya kuwa na gharama ndogo zaidi, imara zaidi kwa ajili kutoa mafuta ya kwanza ya Uganda.

Mradi huu una faida gani?

EACOP lina faida kwa Uganda na Tanzania ambayo inajumuisha utengenezaji wa nafasi za kazi, bidhaa/huduma za ndani (local content), miundombinu mpya, vifaa, uhamishaji wa teknolojia na uimarishaji wa ukanda wa kati (central corridor) wa Uganda na Tanzania.

Faida muhimu ya moja kwa moja ambayo itatoka kwenye bomba la mafuta itakuwa kuongezeka kwa uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni (FDI) kwa serikali zote mbili. Bidhaa/huduma za ndani ni jambo la muhimu kwa washiriki wa mradi wa EACOP na litaunganishwa kikamilifu katika mkakati wa mkataba pamoja na mipango ya mafunzo. Mpango wa bidhaa/huduma za ndani unaandaliwa ili kuongoza mchakato wa utekelezaji.

Inatarajiwa kwamba Bomba litatoa mafunzo kwa watu wanaohusika katika utekelezaji wake, kutoka kwa mafundi wa kuchomea hadi kwa wafanyakazi wa uendeshaji wa bomba, ambao kwa kiasi kikubwa watajumuisha wananchi, wanaopatikana karibu ya eneo la mradi huo.

Kwa kufanya hivyo, ongezeko hili katika uwezo wao litafaidisha makundi haya kwa muda mrefu kwa kuwa wataweza kufanya kazi kwenye miradi kama hiyo au viwanda vingine kwa siku za baadaye.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news