Vijana sita mbaroni kwa kusherehekea kifo cha Hayati Dkt.Magufuli

Vijana sita wilayani Nkasi Mkoa wa Rukwa wanashikiliwa kwa tuhuma za kutoa maneno ya kejeli na kufurahia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt,John Pombe Joseph Magufuli kilichotokea Machi 17, mwaka huu, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI.

Ni wakati akipatiwa matibabu ya matatizo ya mfumo wa umeme katika moyo yaliyokuwa yakiendelea Hospitali ya Mzena mkoani Dar es Salaam

Mkuu wa Wilaya Nkasi, Said Mtanda amesema, vijana hao wamekamatwa Machi 18, mwaka huu baada ya kutolewa taarifa za kifo hicho ambapo vijana hao walikutwa katika vijiji tofauti tofauti wakisherehekea kifo hicho cha Hayati Dkt.Magufuli.

DC huyo amesema,ofisi yake ilipata taarifa juu ya tukio hilo na aliagiza polisi kuwakamata vijana hao ambapo watano walikutwa katika Kijiji cha Malongwe Kata ya Nkandasi na mmoja alikutwa katika Kijiji cha Mkangale mjini Namanyere wakisherehekea huku wakitoa maneno ya kejeli juu ya kifo cha Rais huyo.

Watuhumiwa hao ni Salma Mwananzyungu,Ayubu Sanga,Beatus Kibandiko,Janemerry Lande na Lusajo Lutete wote wakazi wa kKjiji cha Malonje na Charles Vilimani mkazi wa Kijiji cha Mkangale.

Mtanda pia amesema, wanamtafuta kijana mmoja ajulikanaye kwa jina la Pengo ambaye ndiye alikuwa mfadhili wa sherehe hizo ambaye alikimbia baada ya wenzake kukimbia na tayari ameshatoa maagizo kwa Serikali ya kijiji na vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya hatua zaidi.

Post a Comment

0 Comments