MTATIRO AWAFUNDA VIONGOZI KWENYE IFTARI TUNDURU

Na Idd Mohamed,Tunduru

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Julius Mtatiro, ameendelea kukemea tabia ya viongozi kutotumia dhamana walizonazo kupigania haki za wananchi na badala yake wanageuka kuwa mabosi.
DC Mtatiro ameyaeleza hayo alipokuwa anafuturisha mamia ya wananchi wa Tunduru walioalikwa Ikulu Ndogo mjini Tunduru Jumanne 11 Mei 2021.

Mtatiro ameeleza huchukizwa sana na baadhi ya tabia ya watumishi wa umma kushindwa kutatua matatizo ya wananchi kwa wakati na kuanza kuwapiga kalenda bila sababu.

Mtatiro amewakumbusha watumishi wa wilaya yake kuwa, utumishi ni dhamana inayopita haraka, kama siyo kuondolewa, kujiondoa au kustaafu, ziko sababu nyingine nyingi.

Amewataka watumishi wote wakipata nafasi na dhamana ya kuwatumikia watanzania, wafanye hivyo kwa nguvu na uwezo wao wote kwa sababu wananchi wana haki ya kuhudumiwa na kutatuliwa matatizo yao kwa wakati.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news