Uhamisho wa watumishi kufanyika mara nne kwa mwaka

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Prof. Riziki Shemdoe amesema uhamisho wa watumishi wa Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa utafanyika mara nne kwa mwaka yaani kila robo ya mwaka husika, ANARIPOTI MWANDISHI DIRAMAKINI.
Prof. Riziki Shemdoe

Akizungumza na waandishi wa habari Mei 6, 2021 Prof. Shemdoe amesema kila tarehe 10 ya mwezi unaofuata baada ya robo mwaka kwisha uhamisho utafanyika na majina yatawekwa kwenye tovuti ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI.

“Robo kwanza ya mwaka yaan Julai - Septemba majina ya uhamisho yatakua yanatoka tarehe 10 October , na robo ya Pili Oktoba - Desemba majina ya uhamisho yatatoka Januari 10.

"Katika robo ya tatu ya Januari- Machi majina ya uhamisho yatatoka April 10 na robo ya mwisho ya Aprili-Juni majina ya uhamisho yatatoka Julai 10,"amesema.

Aidha, Prof.Shemdoe amebainisha kuwa majina ya watumishi wote watakaohamishwa yatawekwa kwenye Tovuti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI ambayo ni www.tamisemi.go.tz.

Pia amewataka Makatibu Tawala wa Mikoa yote nchini kuwasilisha orodha ya watumishi wa kuhama ofisi ya Rais-TAMISEMI kila tarehe 5 ya mwezi unaofuata baada ya robo mwaka. 

Aidha, amewataka Makatibu Tawala wote kutokupitisha maombi ya watumishi wanaotaka kuhamia kwenye majiji, manispaa na miji kwa kuwa maeneo hayo yana idadi kubwa ya watumishi.

Aidha, Profesa Shemdoe amewataka Makatibu Tawala kuwapa kipaumbele watumishi wenye changamoto mbalimbali zilizothibitishwa.

Pia aliwataka watumishi wote kubaki kwenye vituo vyao na barua za uhamisho zitatumwa kwa waajiri wao na wataona majina yao kwenye Tovuti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Pia amewataka watumishi kujihadhari na matapeli wanaotaka fedha kwa ajili ya kufanikisha uhamisho wao kwa kuwa Uhamisho ni bure na ni haki ya kila mtumishi.

Amesema kuwa, Barua za Uhamisho za kipindi cha nyuma ambazo zilishafika Ofisi ya Rasi TAMISEMI zinashughulikiwa na majina yatatolewa kila mwezi mpaka Juni 30 kabla utaratibu mpya haujaanza kutumika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news