Mfumo wa kielektroniki kutumika kwenye uhamisho wa watumishi

Serikali imesema ipo mbioni kuzindua mfumo wa uhamisho wa watumishi wa halmashauri kwa njia ya kielektroniki ili kurahisisha zoezi la kupitisha maombi ya wanaotaka kuhama kutoka eneo moja kwenda jingine kufanyika kwa uhakika zaidi, anaripoti Mathew Kwembe (Dodoma).
Dkt.Festo Dugange.

Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Korogwe vijijini Mhe.Timotheo Mnzava aliyetaka kujua ni lini Ofisi ya Rais TAMISEMI itazingatia maoni ya Wakurugenzi wa Halmashauri ya kuwapelekea watumishi mbadala kabla ya kuhamisha waliopo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Dkt Festo Dugange amesema serikali imeweka utaratibu wa kuhamisha watumishi wa halmashauri kwa njia ya kielektroniki.

Amesema pindi mfumo huo utakapozinduliwa, maombi yote ya uhamisho wa watumishi wa Mamlaka za serikali za Mitaa yatapitishwa kwa njia ya kielektroniki na yatawezesha kuchuja kwa uhakika zaidi hamisho zote zinazoombwa na kuwezesha watumishi wetu wa maeneo ya vijijini kubaki na kufanya kazi katika maeneo hayo.

Wakati huo huo, Dkt.Dugange amesema, ofisi yake imeendelea kuchuja maombi ya watumishi kwa kuzingatia ikama ya watumishi pindi inapowahamisha kutoka eneo moja kwenda jingine.

Pamoja na kukiri kuwepo kwa changamoto kubwa ya watumishi hao hasa wanaofanya kazi maeneo ya vijijini kutaka kuhamia mijini, Mhe. Dkt. Dugange amesema ofisi yake inahakikisha kuwa inazingatia ikama ya watumishi waliopo.

“Na nimhakikishie Mbunge kwamba si kweli kuwa TAMISEMI imekuwa kila siku inapitisha maombi ya watumishi wote wanaoomba, mara kwa mara tumekuwa tunachuja sababu za msingi ambazo zinapelekea baadhi ya watumishi kukubaliwa lakini walio wengi kutokubaliwa kupata uhamisho,”amesisitiza Naibu Waziri.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news