WAZIRI WA VIWANDA NA WAZIRI WA UWEKEZAJI WAKUTANA NA WAZIRI WA UINGEREZA ANAYESHUGHULIKIA MASUALA YA AFRIKA

Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo na Waziri wa Uwekezaji, Geofrrey Mwambe kwa pamoja wamekutana leo Mei 11, 2021 na kufanya mazungumzo na Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje, Jumuiya ya Madola na Maendeleo ya Uingereza, Bw. James Duddridge.
Katika kikao hicho Mawaziri hao wamepata fursa ya kujadili masuala mbalimbali ya kudumisha na kukuza mahusiano ya biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Uingereza hususani kwa bidhaa muhimu za Tanzania kuuzwa nchini Uingereza na kuvutia Uwekezaji mkubwa wa Uingereza hapa nchini.
Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Prof. Godius Kahyarara pamoja na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. David Concar

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news