Afisa Mazingira alalamikia miradi ya Serikali kutekelezwa pasipo tathimini ya athari ya mazingira Namtumbo

Na Yeremias Ngerangera, Namtumbo

IDARA ya Usafi na Mazingira katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma imeeleza kutoridhishwa juu ya namna ambavyo miradi ya Serikali inavyotekelezwa pasipo tathimini ya athari ya mazingira wilayani humo.

Akisoma taarifa kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Hamad Hassan Chande, Mkuu wa idara hiyo, Kelvin Mnali amesema kuwa, miradi kama ya umwagiliaji,miradi mikubwa ya maji,umeme,ujenzi wa majengo na hata barabara zinatekelezwa pasipo kufanyiwa tathmini ya athari ya kimazingira.

Mnali amesisitiza kuwa, licha ya changamoto ya watumishi wa idara hiyo kuwa ni yeye peke yake hana usafiri wa aina yoyote lakini anajitahidi kwa aina yoyote kutatua changamoto zinazowakabili wananchi kwa wakati.

Alidai zipo changamoto ya uzoaji wa taka katika wilaya ya Namtumbo ambao unakuwa mgumu kutokana na kukosa gari ya kuzolea taka huku akitaja fedha aliyopangiwa katika bajeti ya ofisi yake ni shilingi milioni tatu kwa mwaka kupitia mapato ya ndani kiasi ambacho alidai hakitoshi katika kutekeleza majukumu ya idara hiyo.

Hata hivyo, Mnali alimweleza Naibu Waziri kuwa idara inashirikiana na idara zingine kama TFS,RUWASA ,Ardhi na Maliasili katika uhifadhi wa mazingira vya vyanzo vya maji katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo.

Naye Gravas Mwalyombo ambaye ni Afisa Misitu wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo alimwambia Naibu waziri kuwa, zipo juhudi za dhati za halmashauri za kuhifadhi mazingira ya mto Luegu kutokana na kuwaelimisha wananchi kutenga eneo la chanzo cha mto huo kuwa hifadhi kwa ajili ya matumizi bora ya ardhi na kutunza chanzo cha mto usiharibiwe na shughuli za binadamu.

Mwalyombo alidai Mto Luegu umepita katika hifadhi ya misitu,Hifadhi ya Taifa ya Nyerere,Selous na kukutana na mito mingine katika mkoa wa Morogoro na kupeleka maji yake katika mto Rufiji ambao unajengwa bwawa kubwa la kuzalisha umeme la Mwalimu Nyerere.

Naibu Waziri wa Muungano na Mazingira, Hamad Chande pamoja na mambo mengine aliwaagiza wataalamu wa mazingira na viongozi wa wilaya kuweka mikakati ya maksudi ya kuhakikisha wanaishirikisha jamii katika kulinda chanzo cha mto Luegu pamoja na kingo zake kutovamiwa na kuharibiwa.

Aliagiza wananchi wapewe elimu na waelezwe sheria ya kupisha mto mita 60 na waende mita 100 ili kzifanya kingo za mto Luegu kutoharibiwa katika shughuli za kibinadamu na kuathiri uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali katika bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere ambao unategemea maji kutoka katika mto huo.

Ziara ya Naibu waziri ilikuwa na lengo la kukagua chanzo cha mto luegu ambao umeanzia katika kijiji cha ngwinde kata ya litola na kupita katika kijiji cha Luegu,Mgombasi na Likuyuseka huku mto huo ukichangia asilimia 15 ya mabonde yanayopeleka maji mto rufiji na mto huo huchangia asilimia 18 ya maji yote yanayoingia katika mto Rufuji ambayo ni tegemeo kwa bwawa la kuzalisha umeme la mwalimu Nyerere.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news