Dkt.Senkoro:Mwaka mmoja bila Benjamin Mkapa tunayakumbuka maisha yake na tunaenzi urithi wake

NA BEATRICE SANGA-MAELEZO

Taasisi ya Benjamin William Mkapa kwa kushirikiana na Serikali imeandaa mdahalo wa kumbukizi ya maisha ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamin William Mkapa katika ukumbi wa Mliman City Tarehe 14 July 2021.
Ameyasema hayo Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa, Dkt. Ellen Mkondya-Senkoro, alipokutana na waandishi wa habari leo Julai 10, 2021, katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Dkt. Senkoro amesema, kauli mbiu katika mdahalo huo ni “ Hayati Benjamin Mkapa mwaka mmoja tangu atutoke, tunayakumbuka maisha yake, tunaenzi urithi wake”.

Mtendaji Mkuu ameongeza kuwa, mgeni rasmi katika mdahalo huo atakuwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na baadhi ya viongozi mashuhuri duniani ambao ni Rais wa 42 wa Marekani Mhe. Bill Clinton, aliyekuwa Waziri Mkuu wa uingereza Mhe. Tonny Blair, aliyekuwa Rais wa Nigeria Mhe. Olegesun Obasanjo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Ukimwi (UNAIDS), Winnie Byanyima ambao wote kwa pamoja watatoa salaam zao kwa njia ya video wakielezea walivyomfahamu Hayati Benjamin Mkapa.

“Mdahalo huu utalenga mchango wa hayati Benjamin mkapa ambao ameutoa katika taifa hili,na katika bara la afrika na duniani kwa ujumla ambapo ni pamoja na Afya kwa wote ukiwa ni Urithi wa Rais Benjamin Mkapa katika kujenga Mifumo ya Afya imara na endelevu,” amesema Dkt. Senkoro.

Vilevile wakati wa mdahalo huo Rais Samia atazindua mfuko maalum wa Taasisi “Endowment Fund”. Ambao unaanzishwa chini ya taasisi hiyo wenye lengo la kuongeza chachu katika kuimarisha huduma za afya nchini.

Taasisi ya Benjamin William Mkapa ilianzishwa chini ya Sheria ya Uingizaji ya Wadhamini, Sura ya 375. iliyokusudia kuongeza na kusaidia juhudi za maendeleo za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo uzinduzi wa mpango wake wa kwanza ulijulikana kama "Programu ya Wenzake wa Mkapa" mnamo Julai 2005.

Hayati Benjamin Mkapa alifariki tarehe 23 Julai 2020 jijini Dar es salaam na kuzikwa nyumbani kwao kijiji cha Lupaso Wilaya ya Masasi Mkoa wa Mtwara.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news