NECTA yatangaza shule 10 bora Kidato cha Sita 2021

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Leo Julai 10,2021 Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha sita mwaka 2021 na kutaja shule 10 bora zilizofanya vizuri katika mtihani huo.Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dkt. Charles Msonde amesema shule iliyoshika nafasi ya kwanza ni Kisimiri ya mkoani Arusha iliyokuwa na watahiniwa 72.

Dkt.Msonde amesema, Kemebos ya Kagera yenye watahiniwa 35 imeshika nafasi ya pili ikifuatiwa na Dareda ya Manyara watahiniwa 101.Aidha, nafasi ya nne amsema,imechukuliwa na Tabora Girls yenye watahiniwa 100 ikifuatiwa na Tabora Boys yenye watahiniwa 120.

Dkt.Msonde amesema, nafasi ya sita imeshikwa na Feza Boys ya mkoa wa Dar es Salaam iliyokuwa na watahiniwa 71 ikifuatiwa na Mwandet ya Arusha yenye watahiniwa 53.Matokeo yote soma hapa.

Amesema, Shule ya Zakia Meghji imeshika nafasi ya nane ikitokea mkoani Geita ambayo ilikuwa na watahiniwa 31, ikifuatiwa na Kilosa ya Morogoro yenye watahiniwa 91 na Mzumbe watahiniwa 135.

Post a Comment

0 Comments