Tanzania U-23 yaibuka Mabingwa wa CECAFA Challenge Cup

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Timu ya Taifa ya Tanzania Vijana wenye umri chini ya miaka 23 wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya CECAFA Challenge CUP.

Ni kwa kuifunga timu ya taifa ya Burundi kwa mikwaju ya penati 6-5 baada ya mechi hiyo kumalizika kwa 0-0 ndani ya dakika 90.
Fainali hiyo ambayo ilipigwa katika dimba la Bahir Dar nchini Ethiopia zilishuhudia timu zote zikihitaji ushindi ndani ya dakika 90 bila mafanikio.

Tanzania iliingia fainali baada ya kuichapa timu ya Taifa ya Sudani Kusini bao 1-0 katika mchezo wa nusu fainali wakati Burundi ilipata nafasi ya kuingia fainali baada ya kumfunga Kenya.
Rais wa TFF Wallace Karia (Kulia) na Makamu wa Kwanza wa Rais Athuman Nyamlani (kushoto) wakiwa na Kombe la Ubingwa wa CECAFA Challenge U23 baada ya Timu ya Taifa Tanzania U23 kukabidhiwa ikipata ushindi wa penati 6-5 dhidi ya Burundi kwenye mchezo wa Fainali uliochezwa Ethiopia.

Post a Comment

0 Comments