TFF yawalima faini Simba SC, Yanga SC na Bernad Morrison afungiwa


Bernad Morrison amefungiwa mechi tatu na kutozwa faini ya Shilingi Milioni 3 kwa kosa la kuvua bukta na kubaki na kichupi kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Cup (ASFC) dhidi ya Yanga SC Julai 25, mwaka huu Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.

Taarifa ya TFF leo imesema katika mchezo huo ambao Simba ilishinda 1-0 bao la kiungo Mganda, Thadeo Lwanga dakika ya 80, klabu zote mbili zimetozwa faini kwa makosa mbalimbali ha uvunjaji wa kanuni.

Kiungo Mkongo wa Yanga, Tonombe Mukoko naye amefungiwa mechi tatu na faini ya Sh. 500,000 baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 45 kwa kosa la kumpiga kiwiko mshambuliaji wa Simba, John Bocco.

Kipa Mkenya wa Yanga SC, Farouk Shikalo ametozwa faini ya Sh. 500,000 kwa kosa la kukwepa kusalimiana na waamuzi na wachezaji wa Simba SC.

Post a Comment

0 Comments