Yanga SC yatambulisha nyota wawili wa Kimataifa

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Yanga SC imetambulisha wachezaji wapya wawili.

Wachezaji hao ni beki wa kulia Djuma Shabani na winga wa upande huo huo, Jesus Mololo wote kutoka AS Vita ya kwao, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Jesus Moloko anakuja Yanga kuziba pengo la Mkongo mwenzake, Tuisila Kisinda.

Moloko anayekuja kuziba pengo la Mkongo mwingine, Tuisila Kisinda anayehamia RSB Berkane ya Morocco na kwa pamoja wawili hao wanafanya idadi ya wachezaji watano Yanga kutoka DRC.

Wengine ni kiungo Tonombe Mukoko aliyesajiliwa tangu msimu uliopita pamoja na Kisinda na washambuliaji wapya Fiston Mayele kutoka AS Vita pia na Heritier Makambo kutoka Horoya ya Guinea.
Yanga pia imemsajili makipa wapya wawili, Eric Johola kutoka Aigle Noir ya Burundi na Djigui Diarra kutoka Stade Malien ya kwao, Mali.

Aidha, Yanga SC imesajilu wachezaji wapya wazawa watatu hadi sasa, beki wa kushoto, David Bryson kutoka KMC ya Dar es Salaam, winga wa upande huo huo, Dickson Ambundo kutoka Dodoma Jiji FC ya Dodoma na mshambuliaji Yussuf Athumani kutoka Biashara United ya Mara.

Hata hivyo, Yanga SC inaendelea na utambulisho wa wachezaji wake wapya kabla ya Jumapili kupanda ndege kwenda Morocco .

Ni kwa ajili ya kuweka kambi ya kujiandaa na msimu hadi itakaporejea kwa ajili ya tamasha la Kilele cha Wiki ya Mwananchi Agosti 29, mwaka huu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news