Rais Dkt.Mwinyi, Makamu wa Pili,Mjane wa Maalim Seif wafika kwa Makamu wa Kwanza kumpa pole kufuatia kifo cha kaka yake

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amefika nyumbani kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman, Chukwani Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja kumpa pole kufuatia kifo cha kaka yake marehemu Mwalimu Said Masoud Othman, aliyefariki jana usiku.
Wakati huo huo, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla naye alifika kutoa salamu za pole.
Wakati huo huo, Mjane wa marehemu Maalim Seif Sharif Hamad, Mama Awena Sinani Masoud naye alifika kutoa mkono wa pole
Marehemu Mwalimu Said Masoud, alifariki jana usiku katika hospitali ya rufaa ya Mnazi mmoja kisiwani Unguja, alikolazwa kwa matibabu siku mbili zilizopita.

Mwenyenzi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amen

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news