Watu 206 wathibitika kuwa na Virusi vya UVIKO-19 ndani ya wiki moja

NA MWANDISHI MAALUM-WAF

WAZIRI wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu amesema hali ya UViKO-19 nchini katika kipindi cha tarehe 29 Januari hadi 4 Februari, 2022, jumla ya 6,938 walipimwa na watu 206 walithibitika kuwa na Virusi vya Corona ndani ya wiki moja.
Waziri Ummy ameyasema hayo wakati ya ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Hospitali ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mkoani Mara.

Amesema wagonjwa wapya 71 walilazwa, kati ya hao asilimia 97% walikuwa hawajachanjwa.Na kwa siku ya tarehe 4 Februari, wagonjwa mahututi 11 waliripotiwa na wote sawa na 100% hawakuwa wamepata chanjo dhidi ya UVIKO-19. 

Aidha, amesema wagonjwa watatu (3) wameripotiwa kuwa mahututi na wote (100%) hawajachanjwa. 

Kwa upande wa vifo Waziri Ummy amesema kwa tarehe 29 Januari hadi 4 Februari,2022, Jumla ya vifo vitatu (3) vimeripotiwa kutoka mikoa ya Dodoma (1), Morogoro (1) na Manyara (1), vifo vyote (100%) vilivyoripotiwa vilikuwa vya wagonjwa ambao hawakuchanjwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news