NAIBU WAZIRI SAGINI: TUTAWASHUGHULIKIA ASKARI WANAOCHAFUA JESHI LA POLISI

NA MWANDISHI MAALUM

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini amesema wizara itashughulikia askari wanaochafua Jeshi la Polisi kwa kupitia Tume ya Utumishi wa Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji na Uhamiaji, ili kurejesha imani ya wananchi kwenye vyombo vinavyosimamia ulinzi na usalama wa mali zao.

Amesema kuwa, tume hiyo ni chombo kinachosimamia nidhamu za watumishi wa vyombo hivyo na kwamba Mwenyekiti wa tume hiyo ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Makamu wake ni yeye, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi hivyo watashugulikia kikamilifu maelekezo aliyoyatoa Rais Samia.

“Kuna maelekezo Mheshimiwa umeyatoa, mimi na Waziri Masauni tutayasimamaia kikamilifu. Ipo Tume ya Utumishi wa Jeshi Polisi, Magereza, Uhamiaji na Zimamoto na Uokoaji, chombo hiki ndio kinasimamia nidhamu za watumishi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama,”amesema.
Naibu Waziri Sagini amezungumza hayo mbele ya mamia ya wananchi wa Mara, baada ya kupewa nafasi ya kuongea na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika Hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Kata ya Kwangwa, Musoma Mjini, Mkoani Mara. 

Aidha, Naibu Waziri Sagini amewataka Watanzania kutii sheria na kujiepusha na vitendo vya uhalifu vitakavyowapelekea kuwa wateja wa Vyombo vya Dola. 
Amesema kwamba, vyombo hivyo vinasimamia Sheria na utekelezaji wa sheria na endapo mwananchi atakiuka sheria za nchi basi lazima sheria itachukuliwa.

“Niwaombe wananchi hivi ni vyombo vya dola, Sisi tusingependa vyombo hivi vipambane na raia. Usipokuwa, raia atakaye kikuka sheria, raia atakayetenda vitendo vya uahalifu, atakaye mnyima mwenzake amani atakuwa tuu mteja wa Polisi, na baadae Mahakama, mwishowe Magereza,”amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news